Storm FM
Storm FM
2 July 2025, 12:00 pm

Kushamiri kwa vitendo vya watoto wadogo kutumikishwa kwenye shughuli za bar imewaibua wananchi Sengerema
Na Emmanuel Twimanye:
Wamiliki wa bar katika kata ya misheni Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wamepigwa marufuku kuajiri watoto chini ya umri wa miaka 18 kwa kuwa ni kinyume cha sheria.
Marufuku hiyo imetolewa na Askari polisi kata ya Misheni Insipekta Asha Mohamed wakati akitoa elimu ya masuala ya ulinzi na usalama mahala pakazi kwa wamiliki wa baa katika kata hiyo.
Katika hatua nyingine amewaonya wahudumu wa baa kuacha mara moja tabia ya kugonganisha wanaume ili kuepuka uvunjifu wa amani.
Viongozi wa Serikali ya mtaa na polisi jamii kata ya Misheni wameahidi kufanya msako mkali sehemu za baa ili kukokomesha ajira hatarishi kwa watoto.
Baadhi ya wamiliki wa baa wameahidi kutekeleza suala hilo ili kufanya kazi katika mazingira rafiki.