Storm FM
Storm FM
20 June 2025, 2:55 pm

Wanafunzi kukatiza masomo kwasababu ya kupatiwa ujauzito sasa imekuwa historia kwa wakazi wa kijiji cha Lwamgasa
Na Edga Rwenduru:
Kutokana na changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kutoka kijiji cha Lwangasa kwenda shule ya sekondari Kilombelo Wakazi wa kata ya Lwamgasa Halmashauri ya wilaya ya Geita mkoani Geita wameishukuru serikali kwa kuwajengea shule ya sekondari Isingiro ambayo imepunguza idadi ya utoro kwa wanafunzi.
Wakizungumza na Storm FM kwa nyakati tofauti baadhi ya wazazi na walezi wamesema kuna wakati walilazimika kuingia gharama za kuwapangishia vyumba karibu na shule jambo ambalo lilipelekea watoto wengi wa kike kukatiza masomo kutokana na kubeba ujauzito lakini kwasasa wanaishukuru serikali walisikia kilio chao cha muda mrefu.
Shule ya Sekondari Isingiro ina jumla ya wanafunzi 929 kwa sasa ambapo Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Masaguda Kaminabundo amesema ujenzi wa vyumba vya madarasa mapya zaidi ya kumi vimepunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa wanafunzi katika darasa moja.

Diwani wa Kata ya Lwamgasa Dotto Joseph Kaparatus amesema maendeleo yanayoonekana kwa upande wa sekta mbalimbali katika kata hiyo imetokana na ushirikiano mzuri kati ya serikali na wadau mbalimbali