Storm FM

Vikundi 53 vyapokea mikopo ya milioni 303 Nyang’hwale

3 June 2025, 6:27 pm

Wawakilishi wa vikundi 53 wakipokea mfano wa hundi ya mikopo ya milioni 303. Picha na Mrisho Sadick

Wajasiriamali wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita watakiwa kutumia mikopo ya asilimia 10 kukuza biashara zao

Na Mrisho Sadick:

Serikali wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita imelitaka shirika la maendeleo ya viwanda vidogo (SIDO) kuongeza nguvu ya kutoa elimu , ujuzi na utambuzi wa fursa kwa wajasiriamali hususani maeneo ya vijijini kwani wengi wao wanafanya shughuli za kiuchumi za aina moja ili hali kuna fursa mbalimbali.

Agizo hilo limetolewa na Katibu tawala wa wilaya ya Nyang’hwale Bi Kaunga Amani wakati akikabidhi mikopo ya asilimia 10 yenye thamani ya milioni 303 kwa vikundi 53 vya Wanawake , Vijana na watu wenye ulemavu hafla ambayo imefanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Msalala wilayani humo.

Sauti ya Katibu tawala Nyang’hwale na Meneja wa SIDO
Baadhi ya wanakikundi wakiwa kwenye hafla ya kupokea mikopo ya asilimia 10. Picha na Mrisho Sadick

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi Husna Tony amesema mikopo hiyo imetolewa kwa awamu ya pili huku akivitaka vikundi hivyo kuhakikisha vinakuza biashara zao kupitia mikopo hiyo ili viweze kurejesha nakupewa wahitaji wengine.

Sauti ya Mkurugenzi na Wanakikundi

Halmashauri hiyo bado inapigana vikumbo na vikundi 83 ambayo vinadaiwa marejesho ya zaidi ya milioni 150 huku baadhi ya vikundi hivyo havijulikani wapi vilipo.