Storm FM
Storm FM
29 May 2025, 12:03 pm

Katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Marchi mwaka huu, TAKUKURU mkoa wa Geita imefanikiwa kuokoa jumla ya shilingi 14,221,567 katika miradi minne ya elimu ambayo ilibainika kuwa na mapungufu.
Na: Ester Mabula:
Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari leo Mei 29, 2025, naibu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita Alex Mpemba amesema kiasi hicho kimeokolewa baada ya kubaini dosari mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya kazi yasiyoendana na mabadiliko ya gharama za mradi pamoja na dosari nyingine.
Aidha ameeleza kuwa katika kipindi hicho walipokea jumla ya malalamiko 79 ambapo malalamiko 51 yalihusu makosa ya rushwa na malalamiko 28 hayakuhusu rushwa ambapo uchunguzi unaendelea kwa makosa yanayohusu rushwa.
Katika kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu, ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kusaidia kudhibiti mianya ya rushwa ambapo pia wanaendelea kuelimisha UMMA kupitia semina, mikutano ya hadhara, ufunguzi wa klabu za wapinga rushwa mashuleni pamoja na utoaji wa elimu na habari kupitia vyombo vya habari.
