Storm FM
Storm FM
20 May 2025, 4:17 pm

Mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri imezua kizaa zaa baada ya baadhi ya watu kukosa katika halmashauri ya manispaa ya Geita.
Na: Kale Chongela:
Baadhi ya wananchi kata ya kalangalala, halmashauri ya manispaa ya Geita wamelalamikia kitendo cha kukosa mkopo wa fedha za asilimia kumi inayotolewa na halmashauri kupitia mapato ya ndani licha ya kutuma maombi na kutumia gharama zao ikiwemo kusajili vikundi.
Wakiwa katika ofisi ya kata ya Kalangalala baadhi ya viongozi na wanachama wa vikundi hivyo wamesema walipokea ujumbe wa wito kutoka kwa Afisa mandeleo ya Jamii wa kata hiyo kufika ofisni kwake kuchukua nyaraka zao na barua inayoeleza sababu za kukosa mikopo hiyo ya halmashauri.

Diwani wa kata ya Kalangalala Mhe. Prudence Temba ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi walioomba mikopo hiyo kuwa wavumilivu huku jitihada zikiendelea kufanyika za wao kupewa mikopo hiyo.
Malalamiko hayo yamefika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Geita ambapo ililazimika mkuu wa idara ya maendeleo ya Jamii manispaa ya Geita Ndugu Robert Sugura kuitwa ili kuweza kutoa ufafanuzi juu ya malalamiko hayo.