Storm FM

Bei mpya za mafuta kwa mwezi Mei zinazotumika Geita

8 May 2025, 10:43 am

Roundabout iliyopo katika halmashauri ya manispaa ya Geita.

Kila Jumatano ya kwanza ya mwezi, Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini (EWURA) hutangaza bei mpya kikomo za mafuta ya Petrol, Diesel na Mafuta ya taa.

Na: Ester Mabula:

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini (EWURA) jana Mei 07, 2025 imetangaza bei mpya kikomo za mafuta ambazo zitatumika kwa mwezi Mei.

Katika wilaya za mkoa wa Geita bei hizo mpya ni kama ifuatavyo:

Wilaya ya Geita Petroli itauzwa kwa shilingi 3,113 kwa lita moja kutoka 3,202 mwezi uliopita na Dizeli ni itauzwa kwa shilingi 3,033 kutoka 3,101 mwezi uliopita.

Wilaya ya Bukombe Petroli itauzwa kwa shilingi 3,102 kwa lita kutoka 3,191 mwezi uliopita na Dizeli itauzwa kwa shilingi 3,022 kutoka 3,090 mwezi uliopita.

Wilaya ya Chato Petroli itauzwa kwa shilingi 3,134 kwa lita kutoka 3,223 mwezi uliopita na Dizeli itauzwa shilingi 3,054 kutoka 3,122 mwezi uliopita.

Wilaya ya Mbogwe Petroli itauzwa kwa 3,151 kwa lita kutoka 3,240 mwezi uliopita na Dizeli itauzwa kwa shilingi 3,071 kutoka 3,139 mwezi uliopita.

Wilaya ya Nyang’hwale Petroli itauzwa shilingi 3,128 kwa lita kutoka 3,217 mwezi uliopita na Dizeli itauzwa shilingi 3,048 kutoka 3,116 mwezi uliopita.