Storm FM
Storm FM
23 April 2025, 5:44 pm

‘Kwa sababu tumejitolea kushiriki basi tunaomba serikali itusaidia kuwa na uhakika wa maji na sio kusubiri kipindi cha uchaguzi tu’ – Mwananchi
Na: Kale Chongela:
Wananchi wa mtaa wa Mbabani kata ya Mtakuja, halmashauri ya manispaa ya Geita wamejitolea kufanya usafi katika kisima cha asili baada ya kisima walichokuwa wakitumia kuharibika.
Wakizungumza na Storm FM, baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa maamuzi hayo yamekuja baada ya kisima ambacho walikuwa wakitumia kuharibika jambo ambalo limewapa wakati mgumu juu ya namna ya kupata maji kwaajili ya mahitaji ya kila siku.

Balozi wa eneo hilo Bw. Sijaona Daniel ameeleza kuwa kufuatia usumbufu ambao wananachi walikuwa wanaupitia aliamua ni vyema kuwakusanya ili wasafishe kisima hicho cha asili ambacho kitawasaidia kupata maji
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw. Daud Zahayo amekiri suala hilo kufanyika katika kisima cha asili na kwamba balozi alimpa taarifa ya kuomba kibali cha kualika wananchi ili wajitolee katika kufanya usafi katika eneo ili waanze kupta maji ya kutumia.