Storm FM

Wajasiriamali Mpomvu wapongeza uboreshwaji wa soko

11 April 2025, 2:43 pm

Muonekano wa vibanda vya biashara vinavyotumiwa na wajasiriamali. Picha na Kale Chongela

Soko la Mpomvu linatumiwa na wakazi wa kata ya Mtakuja yenye idadi ya wakazi wapatao 26,676 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022.

Na: Kale Chongela:

Wajasiriamali waliopo katika mtaa wa Mpomvu kata ya Mtakuja katika halmashauri ya manispaa ya Geita wamefurahishwa na maboresho yaliyofanyika ya miundombinu ya ujenzi wa soko.

Wakiwa katika soko hilo leo April 11, 2025 baadhi ya wajasiriamali wameiambia Storm FM kuwa maboresho hayo yamechangia eneo hilo kuwa na muonekano mzuri tofauti na hapa awali kwani walikuwa wakiweka bidhaa zao chini.

Sauti ya wajasiriamali wa soko la Mpomvu

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo ambapo ndipo soko hilo lipo Bw. Charles Manyanga amesema baada ya kukaa na kamati ya serikali ya mtaa huo waliridhia kuanza kuboresha mazingira ya soko hilo kwa kujenga vibanda ili kuwarahisishiwa wajasiriamali kupanga bidhaa zao sehemu nzuri.

Sauti ya mwenyekiti wa Mpomvu Charles Manyanga

Aidha ameongeza kuwa baada ya maboresho hayo kufanyika  mjasiriamlianatakiwa kuendelea kutunza mazingira kwa kufanya usafi eneo linalomzunguka .

Bidhaa mbalimbali katika moja ya banda la mjasiriamali soko la Mpomvu. Picha na Kale Chongela