Storm FM
Storm FM
9 April 2025, 11:44 am

Program maalumu ya utoaji elimu ya kukabiliana na uhalifu kwa makundi mbalimbali ya watu katika Jamii mkoani Geita bado inaendelea tangu ilipozinduliwa Aprili 04, 2025.
Na: Ester Mabula:
Jeshi la polisi mkoani Geita limewataka wananchi kutokubali kukamatwa na mtu yeyote anayedai kuwa ni Askari bila kuonesha kitambulisho ili kukabiliana na changamoto ya watu wanaotumia mwamvuli wa Jeshi hilo kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo utekaji.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisiĀ Safia Jongo jana Aprili 8, 2025 wakati wa mafunzo ya ulinzi shirikishi na polisi jamii, yaliyotolewa kwa watendaji wa kata, vijiji, mitaa, wenyeviti na maofisa tarafa, yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) kwa lengo la kuimarisha usalama wa wananchi.