Storm FM

Wakazi wa kitongoji cha Mhama walia na ubovu wa barabara

8 April 2025, 12:49 pm

Muonekano wa barabara iliyoharibika katika kiongoji cha Mhama, Nampangwe

Kufuatia mvua zinzoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo nchini, zimepelekea changamoto ya miundombinu ya barabara katika baadhi ya maeneo mkoani Geita.

Na: Ester Mabula:

Wananchi wa kitongoji cha Mhama, Kijiji cha Nampangwe, kata ya Runzewe-mashariki  wilayani Bukombe mkoani Geita wameiomba serikali kuwatengenezea barabara inayotoka kijiji cha Nampangwe kuelekea Runzewe mjini kutokana na barabara hio kusombwa na maji hali inayo pelekea wananchi kushindwa kufanya shuguli za kijamii ikiwepo kusafirisha mazao, watoto kushindwa kwenda shule pindi mvua zinaponyesha na wanawake wajawazito kushindwa kufika mapema kwenye kituo cha afya Uyovu kwa ajili ya kupata huduma

Wameeleza hayo April 06, 2025 wakati wakizungumza na Storm FM na kueleza kuwa barabara hiyo imekuwa mbovu tangu mwaka jana 2024 hali ambayo inawapa wasiwasi pindi mvua kubwa zinaponyesha katika eneo hilo

Sauti za wananchi

Mwenyekiti wa kitongoji cha Mhama Yohana Mathias Lupolo katika kijiji cha Nampangwe amekiri juu ya uwepo wa changamoto hiyo na kueleza kuwa wameendelea kuchukua jitihada mbalimbali za utatuzi wa barabara hiyo bila mafanikio ya haraka

Sauti ya mwenyekiti wa kitongoji Yohana Mathias

Diwani wa kata ya Runzewe Mashariki Bi. Mary Chiba akizungumza kwa njia ya simu na Storm FM amekiri kutambua changamoto hiyo huku akieleza kuwa wamechukua jitihada mbalimbali na kwamba matengenezo ya barabara hiyo yataanza mapema mwezi Mei, mwaka huu 2025.

Sauti ya Diwani kata ya Runzewe Mashariki Bi. Mary Chiba