Storm FM

‘Community Policing Outreach program’ yazinduliwa mkoani Geita

4 April 2025, 7:12 pm

Leo April 04, 2025 mkoa wa Geita kupitia Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na GGML umezindua program yenye lengo la kutoa elimu kwa Jamii juu ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

Na: Ester Mabula:

Program hiyo inafadhiliwa na Kampuni ya uchimbaji madini ya GGML iliyopo mkoani Geita ambayo imepewa Kauli mbiu “POLISI JAMII, WAJIBU WETU SOTE”

Mkuu wa kitengo cha Polisi Jamii kutoka GGML Mininjo Edward Tumbo amesema kuwa GGML inaendelea kushirikiana na Jamii inayozunguka mgodi katika nyanya mbalimbali ikiwemo suala la ulinzi na usalama kwani Jamii inapokuwa salama na uzalishaji unakuwa salama.

Sauti ya mkuu wa kitengo cha Polisi Jamii GGML
Mkuu wa kitengo cha Polisi Jamii kutoka GGML Mininjo Edward Tumbo. Picha na Ester Mabula

Akizungumza katika uzinduzi wa program hiyo Kamishna msaidizi wa Jeshi la polisi ACP Elisante Olomi kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma katika Kamisheni ya Polisi Jamii amesema kuwa wanatarajia kupata matokeo chanya kupitia mafunzo hayo ambayo yamelenga kufikia makundi mbalimbali ikiwemo watendaji wa polisi, wananchi pamoja na watendaji kutoka taasisi mbalimbali.

Sauti ya ACP Elisante Olomi
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo. Picha na Ester Mabula

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo amesema moja ya sababu kuu ambazo zilikuwa zinachangia kwa kiasi kikubwa katika matukio ya uhalifu ni pamoja na imani za kishirikina kupitia ramli chonganishi.

Sauti ya SACP Safia Jongo

Mmoja wa wanufaika wa mafunzo yaliyotolewa leo Bi. Rose Paulo amesema kuwa program hiyo itasaidia kuweza kupunguza matukio ya uhalifu ikiwemo migogoro ya ndoa.

Sauti ya mnufaika wa mafunzo
Wanufaika wa mafunzo wakiendelea kufatilia elimu ambayo ilikuwa ikitolewa. Picha na Ester Mabula

Hata hivyo juhudi mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu mkoani Geita ikiwemo mafanikio ya kampeni ya ‘Ongea Nao’ iliyozinduliwa na Jeshi la polisi mkoani Geita ambayo  ilisaidia kupunguza matukio ya mauaji kutoka 49 mwaka 2022 hadi 32 mwaka 2023, sawa na upungufu wa asilimia 34.