Storm FM

Bulldozer lajeruhi watano na kubomoa nyumba 3 Geita

3 April 2025, 6:49 pm

Muonekano wa nyumba iliyobomolewa na mtambo wa uchimbaji. Picha na Edga Rwenduru

“Mazao, miundombinu ya umeme, vimeharibiwa na huu mtambo licha ya kujeruhi watu” – Mwananchi

Na: Edga Rwenduru:

Watu watano kutoka katika kaya tatu zilizopo kitongoji cha Isingilo, kata ya Lwamgasa mkoani Geita wamejeruhiwa vibaya baada ya mtambo unaotumika katika uchimbaji wa madini katika mgodi wa dhahabu wa Buckreef kugonga na kuharibu nyumba tatu za wakazi wa kitongoji hicho.

Mashuhuda ambao pia ni waathirika wa tukio hilo Charles Mhoja na Mariam Kasandiko wamesema licha ya kujeruhi watu pia limesababisha uharibifu wa nyumba, miundombinu ya umeme ,mazao pamoja na chakula.

Sauti ya mashuhuda

Mwenyekiti wa kijiji cha Lwamgasa Mwita Chacha Amos amesema kwa taarifa alizozipata ni kwamba trekta hilo lilitoka maeneo ya mgodi likiwa halina dereva anayeliongoza 

Sauti ya mwenyekiti Chacha Amos

Akitolea ufafanimuzi wa nini sababu ya kutokea kwa tukio hilo Afisa habari wa Mgodi wa Bakreef Amelda Msuya amesema ajali hiyo imesababishwa na Dereva yaani Operator aliyekuwa akijaribu kuiba mafuta.

Sauti ya Afisa habari wa Buckreef Amelda Msuya
Wananchi mbalimbali wakiwa eneo la tukio kushuhusia uharibifu. Picha na Edga Rwenduru
Mtambo aina ya Grader ambao umepelekea majeruhi na uharibifu wa mali. Picha na Edga Rwenduru