

31 March 2025, 4:18 pm
Michezo ni nguzo muhimu katika kuimarisha mahusiano na kuongeza uwajibikaji kazini kwa watumishi wa umma.
Na Mrisho Sadick:
Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita Grace Kingalame amewataka watumishi wa serikali Mkoani Geita kutumia michezo kuondoa tofauti zao nakuweka mbele maslahi ya wananchi.
Kingalame ametoa kauli hiyo kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela katika bonanza lililowakutanisha watumishi wa serikali wa Mkoa wa Geita katika viwanja vya shule ya msingi Waja Manispaa ya Geita.
Afisa michezo wa Mkoa wa Geita Bahati Rodgers amesema bonanza hilo lilikuwa na michezo zaidi ya 20 huku baadhi ya washiriki wakipongeza kuanzishwa kwa michezo hiyo kila robo ya mwaka.
Mrisho Sadick anakuja na undani wa taarifa hii