

29 March 2025, 1:47 pm
Kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba nchini Tanzania, viongozi wa dini ya Nyanguku wameungana kuliombea Taifa.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Viongozi wa dini mbalimbali katika kata ya Nyanguku iliyoko halmashauri ya manispa ya Geita wamekutana kwaajili ya kuliombea taifa la Tanzania kuelekea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mapema mwaka huu.
Maombi hayo yamehudhuriwa na Diwani wa kata ya Nyanguku ambaye pia ni naibu Meya Manispaa ya Geita Elias Ngole ambapo amesema kuwa viongozi wa dini wamekuwa mstari wa mbele katika kuchagiza amani na upendo katika nchini huku akiwapongeza kwa maono yao ya kuona umuhimu wa kuwa na umoja wa viongozi wa dini katika kata hiyo.
Viongozi wa dini katika kata ya Nyanguku wamebainisha malengo yao makuu ya kuanzisha umoja huo.
Aidha viongozi hao wameomba serikali za vijiji na vitongoji katika kata hiyo kufanya mikutano ya serikali siku nyingine tofauti na siku za ibada.
Afisa mtendaji wa kata ya Nyanguku Angel Zahoro ametolea ufafanuzi jambo hilo ambalo limeombwa a viongozi wa dini.