Storm FM

Wajasiriamali wahofia bei ya nyanya kupanda Manispaa ya Geita

29 March 2025, 1:35 pm

Eneo ambalo wajasiriamali hulangua nyanya katika soko la Asubuhi Nyankumbu

Bei ya nyanya imepanda katika halamshauri ya manispaa ya Geita tofauti na ilivyokuwa mwezi uliopita hali ambayo inapelekea wasiwasi kwa watumiaji na wauzaji.

Na: Kale Chongela – Geita

Wajasiriamali  waliopo katika soko la asubuhi Nyankumbu katika halmashauri ya manispaa ya Geita  wamehofia mitaji yao kukata kutokana na nyanya kupanda bei.

Wakizungumza na Storm Fm Machi 28, 2025 baadhi ya wajasiriamali hao wamesema kwa sasa nyanya zimepanda bei kutoka shilingi elfu 20 hadi shilingi elfu 75.

Sauti ya wajasiriamali

Licha ya baadhi ya wajasiriamali kuhofia mitaji yao kwa upande wa wakulima wao wamedai kunufaika na hali hiyo kwani wameanza kuuza kwa bei ya juu tofauti na hapa awali.

Sauti ya wakulima

Mwenyekiti wa wauza nyanya katika soko la asubuhi Nyankumbu Bw. John Malimi amekiri nyanya kupanda bei na kueleza kuwa ipo haja ya kila mjasiriamali kusoma nyakati na majira ili kuendelea kulinda mitaji yao.

Sauti ya mwenyekiti