

19 February 2025, 10:50 am
Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Geita, zimepelekea baadhi ya athari za kimiundombinu kwa baadhi ya wananchi katika manispaa ya Geita.
Na: Kale Chongela – Geita
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Mbugani, kata ya kalangalala, halmashauri ya manispaa ya Geita makazi yao yameathiriwa na mvua ilyoambatana na upepo mkali hali iliyosababaisha nyumba kuezuliwa .
Wakizungumza na Storm FM baadhi ya wananchi wa eneo hilo walioharibiwa makazi yao wamesema mvua hiyo ilinyesha Februari 17, 2025 majira ya jioni na wakat ikiendelea kunyesha ghafla upepo ulivuma na kuezua mabati
Balozi wa eneo hilo Bw. Joseph Mayila ameeleza namna alivypata taarifa juu ya tukio hilo
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw. Jumanne Jason amekiri kutokea kwa uharibifu huo na kufafanua kuwa kamati ya maafa wilaya ya Geita imefika eneo hilo ikiongozwa na katibu tawala wilaya ya Geita