

10 February 2025, 4:41 pm
Meli ya MV Jubilee hope imekuwa ikitoa huduma za afya kwa jamii inayozunguka visiwa mbalimbali vya Ziwa Viktoria.
Na: Ester Mabula – Geita
Kampuni ya Geita Gold Minning Limited (GGML) imeendelea kujivunia jukumu lao la kudhamini huduma za afya zinazotolewa na meli ya MV Jubilee Hope. Meli hiyo imekuwa ikitoa huduma za afya kwa jamii inayozunguka visiwa mbalimbali vya Ziwa Viktoria.
Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha muongo mmoja wa utoaji huduma hiyo, Makamu wa Rais wa wa masuala ya uendelevu wa AngloGold Ashanti- Afrika, Simon Shayo, amesema kuwa kampuni inatambua na kuthamini umuhimu wa sekta ya afya na itaendelea kudhamini uwepo wa meli hiyo ili kutoa huduma kwa wananchi
Kwa upande wake, mkurugenzi wa usalama na utunzaji wa mazingira kutoka TASAC, Letcia Mtaki, amesema ushiriki wao katika mradi huo ni kuendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye meli ili kuhakikisha usalama wa chombo hicho.
Kampuni ya GGML tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000 imeendelea kuwa mshirika muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia miradi mbalimbali ya CSR katika sekta za afya, elimu na miundombinu katika maeneo yanayozunguka mgodi huo.