Storm FM

Ubora wa miradi waikosha CCM Nyangh’wale

31 January 2025, 11:01 am

Kamati ya siasa ya CCM wilayani Nyagh’wale ikiwa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo. Picha na Mrisho Sadick

Miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani Nyangh’wale Mkoani Geita imewaibua CCM kutokana na utekelezaji wake kufuata taratibu zote za ujenzi.

Na Mrisho Sadick:

Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita imetembelea nakukagua miradi ya Afya na Elimu iliyotekelezwa kwa thamani ya zaidi ya milioni 900 huku ikiridhishwa na utekelezaji wake.

Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyang’hwale Al Haji Adam Mtore ikiwa katika Ziara yake ya siku ya kwanza ya kukagua miradi ya maendeleo imeanza kutembele Nyumba ya walimu katika shule ya msingi Iparang’ombe , ukamilishaji wa madarasa manne shule ya sekondari Nyabakamba kisha ujenzi wa mabweni mawili ya na madarasa matano katika shule ya sekondari Bukwimba.

Akitoa taarifa mbele ya kamati hiyo afisa mtendaji wa Kata ya Bukwimba Sijosphat Mlilie amesema miradi ya ujenzi wa mabweni na madarasa inagharimu zaidi ya milioni 300 nakwamba utekelezaji wake umefikia 60% na ikikamilika yoye kwa pamoja itawanufaisha wanafunzi zaidi ya 320 huku Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Nyangh’hwale Said Madoshi amewapongeza viongozi wa wilaya hiyo kwa usimamizi mzuri wa miradi huku akiwasisitiza kuendelea kuongeza kasi ili wananchi waweze kufurahia matunda ya serikali yao.

Sauti ya mtendaji na Katibu mwenezi CCM Nyangh’wale
Muonekano wa baadhi ya madarasa ya shule mpya ya sekondari kanegele wilayani Nyangh’wale. Picha na Mrisho Sadick

Sambamba na miradi hiyo kamati hiyo imetembelea mradi wa ujenzi wa Nyumba ya watumishi katika Kituo Cha Afya Kafita, ujenzi wa mabweni mawili katika shule ya sekondari Kanegele huku Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Grace Kingalame na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo wakaahidi kufanyia kazi dosari ndogo ndogo zilizobainika kwa baadhi ya miradi wakati wa ukaguzi huo.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Nyangh’wale

Akiwa kwenye ukaguzi wa mradi wa mwisho katika shule ya sekondari Kanegele Mwenyekiti wa CCM Adam Mtore mbali nakuwapongeza viongozi wa wilaya ya Nyang’hwale kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufanya makubwa wilayani humo.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyangh’wale Adam Mtore akizungumza na watendaji wa serikali baada ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani humo. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Mwenyekiti wa CCM Nyangh’wale