Msaada wa kisheria wa Mama Samia wafika Nyabulanda Geita
29 January 2025, 12:45 pm
Wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani Geita wameendelea kupokea msaada wa kisheria juu ya masuala mbalimbali kupitia kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia Lega Aid.
Na: Kale Chongela – Geita
Wakazi wa kata ya Nyabulanda wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita wamepewa elimu juu ya umiliki halali wa ardhi ili kuondokana na migogoro isiyokuwa ya lazima sambamba na kupoteza haki zao.
Elimu hiyo imetolea na afisa ardhi halmashauri ya Nyang’hwale Bw. Goodluck Masatu Januari 27, 2025 akiwa katika kijiji cha Bujula katika mwendelezo wa kampeni inayoendelea ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal AID ambapo wananchi wameeleza namna walivyopokea elimu hiyo.
Afisa ardhi halmashauri ya Nyang’hwale Bw. Goodluck Masatu ameeleza manufaa watakayopata wananchi kupitia elimu hiyo na kubainisha hatua halali za kumiliki ardhi.
Afisa mtendaji wa kata ya Nyabulanda Bw. Alphonce Malando ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali kwa kusogeza huduma ya msaada wa kisheria na kueleza namna migogoro ya ardhi inavyosumbua wananchi wake kutokana na kukosa elimu ya kisheria.