Wazazi walia na changamoto ya madawati Mtakuja
20 January 2025, 12:41 pm
Licha ya juhudi za serikali kuhakikisha inajenga vyumba vya madarasa nchini, bado wakazi wa kijiji cha Mtakuja wanaeleza changamoto wanayopitia.
Na: Nicholaus Lyankando – Geita
Wanafunzi katika shule ya msingi Mtakuja kata ya Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita wamelazimika kusoma wakiwa wamekaa chini kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati katika shule hiyo.
Wakizungumzia changamoto hiyo baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 1000 ikiwa na vyumba vinne tu vya madarasa wameeleza kupitia wakati mgumu hasa katika kipindi cha kujisomea
Wazazi na walezi katika kijiji hicho nao wameungana na watoto wao kuendelea kuiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto hiyo.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Abdalah Nkingwa ameeleza mikakati waliyochukua katika kukabiliana na changamoto hiyo.
Hata hivyo Afisa elimu kata ya Lulembela Nchambi Samson amekiri juu ya uwepo wa changamoto hiyo na kuahidi kuanza utekelezaji wa kuitatua changamoto hiyo.