Wakazi wa Nshinde washukuru kujengewa shule
6 January 2025, 3:47 pm
Kufuatia changamoto ya muda mrefu ya kutokuwa na shule ya msingi katika mtaa wa Nshinde, hatimaye serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imkamilisha ujenzi wa shule katika mtaa huo.
Na: Kale Chongela – Geita
Wakazi wa Mtaa wa Nshinde kata ya Nyankumbu mjini Geita wameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu kwa kuwajengea shule ya msingi katika eneo hilo.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wananchi wa mtaa wa Nshinde kata ya Nyankumbu leo Januari 06, 2025 ambapo wameiambia Storm FM kuwa shule hiyo imekuwa msaada mkubwa katika kutatua changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwaajili ya kusoma katika shule za maeneo jirani.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Nshinde Bw. Edward Malimi amesema shule hiyo itaanza kupokea wanafunzi mhula wa kwanza 2025 pindi shule zitakapofuguliwa huku akiwasihi wazazi na walezi kuanza kufanya maandalizi mapema ya wanafunzi.
Diwani wa kata ya Nyankumbu Bw. John Lunyaba Mapesa amesema serikali ya awamu ya sita inayoongazwa na Dkt. Samia Suluhu imeendelea kujenga miradi mbalimbali ya elimu katika kata hiyo na kwamba shule hiyo imegharimu zaidi ya Tsh. milioni 350.