Storm FM
Storm FM
6 December 2024, 8:22 am

Ni moja ya eneo lililopo mtaa wa Ibolelo, kata ya Nyankumbu mjini Geita ambalo limeathirika na mvua, Je wananchi wanaishi vipi katika mazingira haya?.
Na: Ester Mabula – Geita
Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Geita zimeendelea kuleta changamoto kwa wakazi wa mjini Geita baada ya nyumba kadhaa kuzingirwa na maji huku baadhi ya vyoo na visima vikifurika maji katika mtaa wa Ibolelo maarufu kwa jina la Mwabasabi uliopo kata ya Nyankumbu katika Halmashauri ya Mji wa Geita.

Akizungumza na Storm FM kwa niaba ya wananchi wengine, Bi Leticia Paulo amesema mvua iliyonyesha jana Disemba 06, 2024 majira ya asubuhi ndio imesababisha maji kujaa katika makazi yao hali iliyowapelekea wananchi hao kushindwa kuendelea na shughuli zao za kila siku huku wakihofia usalama wa mali na Afya zao.
Mwenyekiti wa Kamati ya miundombinu mtaa huo Nzeleli Nyalukamo amesema wameungana na wananchi kuzibua mitaro na kufungua barabara ili maji yaliyotuama yaweze kutoka kwani halmashauri haijawasaidia kutatua changamoto hiyo.