Storm FM

Binti aliyevunjika uti wa mgongo Inyala awashukuru

19 November 2024, 8:33 pm

Maendeleo ya Annastazia Jackobo mkazi wa kijiji cha Inyala Kata ya Nyamigota baada ya kutoka Bugando Jijini Mwanza. Picha na Mrisho Sadick

Nguvu ya umma imeendelea kurejesha tabasamu kwa Annastazia aliekata tamaa ya maisha nakutamani afe baada ya kuvunjika uti wa mgogo wakati akichuma maembe juu ya mti

Na Mrisho Sadick:

Annastazia Jackobo mkazi wa kijiji cha Inyala Kata ya Nyamigota wilayani na Mkoani Geita aliyevunjika uti wa mgongo baada ya kuanguka kutoka juu ya mti wa mwembe nakukaa ndani kwa zaidi ya miaka miwili bila kupata msaada wowote, amewashukuru watanzania hususani wakazi wa Mkoa wa Geita kwa kujitoa kumchangia nakufikia hapo alipo kwasasa.

Storm FM Sauti ya Geita ilipata taarifa za uwepo wa binti huyo miezi mitatu iliyopita ambae alitelekezwa na mume wake baada ya tatizo hilo, alikuwa na hali mbaya kwani baada ya kuvunjika uti wa mgongo alikuwa hawezi hata kujigeuza hali iliyosababisha kupooza miguu yake , kupata vidonda vikubwa sehemu za makalio , kushindwa kuzuia haja kubwa na ndogo.

Maendeleo ya Annastazia Jackobo mkazi wa kijiji cha Inyala Kata ya Nyamigota baada ya kutoka Bugando Jijini Mwanza. Picha na Mrisho

Hali hiyo iliisukuma Storm FM kuanzisha kampeni maalumu ya kumsaidia Annastazia kwa kuwaomba watanzania wakiwemo wakazi wa mkoa wa Geita na wadau mbalimbali kumchangia fedha kwa ajili ya kwenda kupata matibabu ya kibingwa, safari ya matumaini kwa Binti huyu anaeishi na mama yake mzee ambae hajiwezi ikaanza kuonekana.

Watanzania waliguswa na changamoto za binti huyo nakuanza kujitolea kuchangia kwa utaratibu uliowekwa na Storm FM hali iliyowezesha kufikishwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na baadae Bugando Jijini Mwanza ambako alikaa zaidi ya mwezi mmoja, baada ya Annastazia kutoka Bugando akiwa na hali ya matumaini mapya ameiambia Storm FM kuwa alikuwa amekata tamaa hali ambayo alitamani hata afe kwakuwa alikuwa hawezi kufanya chochote, anawashukuru watu wote waliojitokeza kumsaidia ikiwemo Storm FM ambayo ilibeba ajenda hii nakuifikisha kwa watanzania amesema Mungu awabariki lakini bado anakabiliwa na changamoto nyingi kwa mtu ambae atawiwa kumsaidia unakaribishwa.

Sauti ya Annastazia
Maendeleo ya Annastazia Jackobo mkazi wa kijiji cha Inyala Kata ya Nyamigota baada ya kutoka Bugando Jijini Mwanza. Picha na Mrisho

Mkurugenzi mtendaji wa Storm FM Modesta Olga Mselewa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali waliibeba ajenda hii kwa hali na mali nakufanikisha binti huyo kupelekwa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na baade Bugando jijini Mwanza licha ya ugumu na ukata wa fedha uliokuwepo lakini hakuna mtu aliekata tamaa kama anavyo eleza Bi Modesta.

Sauti ya Mkurugenzi Storm FM

Nambari ya mawasiliano na msaada zaidi ni 0756 39 70 26.