Storm FM

Huduma ya mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu yazinduliwa Chato

11 November 2024, 1:08 pm

Katibu tawala wa mkoa wa Geita wapili kutoka kulia akijione huduma za mifuta zilizosogezwa katika Hospitali ya rufaa ya kanda Chato. Picha na Edga Rwenduru

Hospitali ya rufaa ya kanda Chato imeendelea kusogeza huduma za kibingwa ili kuwapunguzia mzigo wananchi wa kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma hizo.

Na Edga Rwenduru:

Kutokana na changamoto ya muda mrefu ya wananchi wa mkoani Geita na mikoa jirani kusafiri umbali mrefu kwenda Jijini Dar es salaam  kufuata huduma ya matibabu ya mifupa,ubongo na Mishipa ya fahamu  Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Chato kwa kushirikiana na hospitali ya MOI imezindua huduma hizo za kibingwa ili kutatua changamoto hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hizo za kibingwa uliofanyika katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya Chato Dkt Oswald Lyapa mkurugenzi wa huduma za matibabu wa hospitali hiyo amesema uzinduzi wa huduma hizo umelenga kuwaondolea adha wananchi wa mkoa wa Geita ,Kagera na Kigoma ambao wilikuwa wanalazimika kutumia gharama kubwa kufuata huduma hizo hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza.

Sauti ya Dkt Osward Mkurugenzi wa huduma za matibabu Chato

Baadhi ya wananchi wamebainisha jinsi huduma hizo za kibingwa zitakavyo kwenda kuwasaidia kwani hapo awali walikuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta huduma hizo hali ambayo iliwafanya wengine kushindwa kutokana ugumu wa maisha nakusababisha kuwapoteza wapendwa wao.

Sauti ya wananchi Chato
Picha ya pamoja viongozi , madaktari na wananchi baada ya zoezi la uzinduzi wa huduma za mifupa Chato. Picha na Edga Rwenduru

Katibu tawala wa mkoa wa Geita Mohamed Gombati ambaye amezindua huduma hiyo  ya matibabu ya kibingwa amewataka watumishi kutoa huduma kwa kuzingatia weledi wa kazi yao ili kuwasaidia wananchi wanaotoka maeneo mbalimbali kwa ajili ya kupata huduma hapo.

Sauti ya katibu tawala Mkoa wa Geita
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za kibingwa katika Hospitali ya rufaa ya kanda Chato. Picha na Edga Rwenduru