Kampeni ya ‘Tuwaambie kabla hawajaharibiwa’ ilivyozinduliwa Geita
24 September 2024, 3:37 pm
Imeelezwa matukio ya ukatili ikiwemo vitendo vya ubakaji yameongezeka mkoani Geita kwa mwaka 2024 kufikia 91 kutoka 71 mwaka 2023.
Na: Kale Chongela – Geita
Wananchi mkoani Geita wametakiwa kuendelea kutoa ushirikiano juu ya vitendo vya ukatili ikiwemo upakaji ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi SACP Safia Jongo Septemba 22, 2024 akiwa katika shule ya msingi Uwanja kata ya Nyankumbu mjini Geita kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupinga vitendo vya ukatili.
Kamanda Jongo amesema kwa mwaka 2023 matukio ya ubakaji yalikuwa 71 ambapo mwaka huu 2024 yameongezeka na kufikia matukio 91.
Msimamizi wa masuala ya kijinsia kutoka shirika la Plan Internation mkoani Geita Bi. Hildegada Mashauri amesema kila mmoja analo jukumu ya kumlinda mtoto ili atimize ndoto zake.
Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela ambaye alikuwa mgeni rasmi ametumia fursa hiyo kuwataka wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao juu ya matumizi ya simu kwani baadhi yao wanajifunza matendo yasiyofaa kupitia simu zao.