Storm FM

Changamoto ya taka Geita mjini bado kizungumkuti

11 September 2024, 10:24 am

Utupaji wa taka hovyo katika mtaa wa Msalala Road. Picha na Amon Bebe

Changamoto ya taka Geita mjini bado ni kitendawili wananchi watajwa kuwa kikwazo kwa kushindwa kupeleka taka hizo sehemu husika.

Na Amon Bebe:

Licha ya uwepo wa gari linalopita mtaani kukusanya taka katika Halmashauri ya Mji wa Geita mkoani Geita baadhi ya wananchi wanadaiwa kutopeleka uchafu kwenye gari hilo hali inayochangia kutapakaa kwa taka maeneo mengi.

Wakizungumza na Storm FM baadhi ya wakazi wa mtaa wa Msalala Road Mashariki wamesikitishwa na kitendo cha baadhi ya wananchi wenzao kusambaza taka hovyo katika mitaa yao na huku gari linapita kila siku kukusanya uchafu.

Utupaji wa taka hovyo katika mtaa wa Msalala Road. Picha na Amon Bebe
Sauti ya wakazi Msalala Road

Nao baadhi ya wananchi wanaotuhumiwa kufanya vitendo vya utupaji wa taka hovyo mitaani ambao asilimia kubwa ni wauzaji wa pombe za kienyeji, wamekana kufanya hivyo huku wakisema wanaonewa na endapo ni kweli basi wawakamate na kuwachukulia hatua.

Sauti ya wakazi wa Msalala Road

Afisa afya na mazingira wa Halmashauri ya Mji wa Geita Edward Mwita amewataka wananchi kutumia gari la ukusanyaji wa taka linalopita mtaani kwao nakwamba kwa mtu atakae kiuka utaratibu huo atachukuliwa hatua za kisheria.

Sauti ya afisa mazingira Geita mji