Storm FM

Mapato ya madini ujenzi, Geita Mji yapaa

15 August 2024, 2:30 pm

Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya mji wa Geita wakiwa katika kikao cha baraza. Picha na Mrisho Sadick

Madini ujenzi ikiwemo mawe , kokoto , mchanga na moramu chanzo cha mapato kilichokuwa hakitazamwi sana katika halmashauri ya mji wa Geita.

Na Mrisho Sadick:

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Geita mkoani Geita limempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo kwa kuongeza kiwango cha makusanyo ya mapato kwenye madini ujenzi kwa kipindi cha mwezi julai.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita  Elias Ngole akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani Agosti 14,2024 amempongeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kuongeza mapato kutoka katika chanzo cha madini ujenzi huku akimtaka kuendelea kupambana zaidi.

Kulia ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita Costantine Morandi na kushoto ni makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Elias Ngole. Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya Makamu Mwenyekiti Geita mji

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Yefred Myenzi amesema kwa kipindi cha mwezi juni hadi julai wamekusanya zaidi ya milioni 20 kutoka milioni 2 iliyokuwa ikikusanywa hapo awali  katika madini ujenzi huku siri ya mafanikio hayo ameeleza kuwa ni pamoja na kuongeza udhibiti.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Geita Yefred Myenzi akizungumza na Stporm FM . Picha na Mrisho Sadick
Sauti ya mkurugenzi Geita mji

Katika hatua nyingine Myenzi amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025 halmashauri hiyo imepanga kukusanya zaidi ya bilioni 20 ikiwa ni sehemu ya bajeti ya halmashauri hiyo huku akiahidi kuendelea kubuni vyanzo vipya ili kuongeza mapato zaidi.

Sauti ya mkurugenzi Geita mji

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Costantine Morandi amesema licha ya halmashauri hiyo kupokea pesa zaidi ya bilioni 1 kutoka serikali kuu kwa ajili ya shughuli za maendeleo amemtaka mkurugenzi kuendelea kuongeza nguvu ya makusanyo ya mapato ya ndani nakukamilisha miradi mbalimbali kwa manufaa ya wananchi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri mji wa Geita