Storm FM

Binti ajifungua na kutupa kichanga chooni Geita

6 August 2024, 3:33 pm

Choo cha familia ambacho mtoto mchanga alitupwa baada ya kuzaliwa. Picha na Evance Mlyakado

Kituo cha redio cha Storm FM kilichopo mkoani Geita kinaendesha kampeni ya kupinga vitendo vya ukatili iitwayo INATOSHA PINGA UKATILI yenye lengo la kupaza sauti kwa jamii kuachana na vitendo vya ukatili.

Na: Evance Mlyakado – Geita

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Binti aliyetambulika kwa jina la Nyabuso Lukansora Majura anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 mkazi wa kijiji cha Ihumilo kata ya Nkome halmashauri ya wilaya ya Geita anadaiwa kujifungua na kisha kutupa kichanga ndani ya shimo la choo kinachotumiwa na familia yao.

Baba mzazi wa binti huyo amesema kuwa Agosti 04, 2024 majira ya saa 2 usiku akiwa ametoka eneo la nyumbani alipigiwa simu na kijana wake wa kiume akimueleza kuwa ndani ya choo chao kumetapakaa damu hali iliyomfanya kurudi nyumbani ili kufahamu zaidi kilichotokea na ndipo akakuta tukio hilo.

Sauti ya baba mzazi
Lukansora Majura, baba mzazi wa binti anayedaiwa kutupa mtoto ndani ya shimo la choo. Picha na Evance Mlyakado

Mwenyekiti wa kijiji cha Ihumilo, Tumaini Christopher amesema serikali ya kijiji kwa kushirikiana na jeshi la polisi na wataalamu wa Afya kata ya Nkome wamefanikiwa kutoa kichanga hicho ndani ya shimo la choo kikiwa tayari kimekwisha poteza uhai.

Sauti ya mwenyekiti

Baadhi ya majirani na wananchi wa kijiji hicho wameeleza jinsi walivyofanikiwa kupata taarifa za tukio hilo huku wakibainisha baadhi ya sababu ambazo huenda zikawa zimepelekea binti huyo kufanya kitendo hicho.

Sauti ya majirani
Binti anayediwa kutupa mtoto kwenye shimo la choo baada ya kujifungua. Picha na Evance Mlyakado