Wakazi Nyakagomba wajengewa mnara wa mawasiliano
18 July 2024, 3:19 pm
Serikali imejipanga kuboresha miundombinu ya mawasiliano itakaowezesha wananchi waishio maeneo ya vijijini kupata huduma ya mtandao.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Wakazi wa kata ya Nyakagomba Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita wameondokana na changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa huduma ya mtandao baada ya serikali kutoa ruzuku ya ujenzi mnara wa mawasiliano ya simu katika eneo hilo.
Nzunga Solele, Zacharia Magesa na Masalu Marco ni wakazi wa kata hiyo ambapo wakizungumza wakati wa ziara ya waziri habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Nnauye ya kukagua ujenzi wa mnara uliojengwa katika eneo hilo wamesema kabla ya ujenzi wa mnara huo walikuwa wanapanda mlimani kwaajili ya kupata huduma ya mtandao.
Mbunge wa Busanda Mhandisi Tumaini Magesa pamoja na Mkuu wa mkoa wa Geita mhe. Martine Shigela wamesema mnara huo umeghalimu zaidi ya shilingi milioni 100.
Waziri Nape Nauye amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kila eneo linakuwa na huduma ya mtandao ili kurahisisha mawasiliano.