Storm FM

Afisa elimu sekondari mjini Geita atoa wito kwa wazazi

13 July 2024, 1:10 pm

Moja ya shule zilizopo mjini Geita (Picha kutoka maktaba na Storm FM).

Halmashauri ya Mji wa Geita yenye wanafunzi 25,155 ina shule za sekondari 16 ikiwa ni ongezeko la shule mpya 16 kutoka shule 10 zilizokuwepo mwaka 2019.

Na: Kale Chongela – Geita

Wazazi na walezi halmashauri ya mji wa Geita wametakiwa kuendelea kutimiza majukumu yao kwa wanafunzi ili kuwawezesha kuongeza ufaulu kwenye masomo.

Wito huo umetolewa na afisa elimu sekondari  halmashauri ya mji wa Geita Richard Mhaya Julai 12, 2024 ofisini kwake wakati akizungumza na Storm FM ambapo amesema miongoni mwa jukumu kubwa kwa mzazi/mlezi ni pamoja na  kujenga desturi ya kufanya ufuatiliaji wa masomo ya mwanafunzi.

Sauti ya afisa elimu sekondari

Baadhi ya wazazi mjini Geita wamebainisha kuwa licha ya jitihada ambazo wamekuwa wakifanya pia suala la utafutaji riziki limekuwa likibadili mfumo wa maisha.

Sauti ya wazazi

Aidha wameongeza kwa kusema ili kuhakikisha ufaulu unaendelea kukua kwa kiwango kikubwa ipo haja ya walimu na wazazi kushirikiana kwenye malezi ya pamoja kwa mtoto.