Storm FM

Matibabu bure kwa wazee bado kizungumkuti

1 July 2024, 3:47 pm

Sera ya matibabu bure kwa wazee nchini bado inagubikwa na vikwazo mbalimbali ambapo walengwa ambao ni wazee mkoani Geita wameeleza changamoto wanazopitia.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Baadhi ya wazee wanaoishi katika kata za Kalangalala, Mtakuja na Bombambili katika halmashauri ya mji wa Geita wamelalamikia vituo vingi vya kutolea huduma za afya kutokuwa na madirisha maalum kwa ajili ya wazee licha ya serikali kuelekeza kila kituo cha kutolea huduma ya afya kuwa na madirisha hayo.

Wazee wakiwa katika hafla maalum iliyoandaliwa na TAGCO katika ukumbi wa Gedeco. Picha na Edga Rwenduru

Kilio hicho kimetolewa na wazee hao wakati wa hafla maalum iliyoandaliwa na Shirika la Kuwalea Wazee Wanaoishi Mazingira Magumu (Tanzania Grandparents Care Organization)TAGCO hafla ambayo imefanyika katika ukumbi wa GEDECO uliopo mjini Geita kwa lengo la kuwapatia mahitaji muhimu wazee zaidi ya 60 wanaoishi mazingira magumu.

Clemence Audax, Katibu Mkuu Mtendaji TAGCO. Picha na Edga Rwenduru

Clemence Audax ni katibu mkuu mtendaji wa shirika la TAGCO amesema wazee wote wanaohudumiwa na shirika hilo watakuwa wanapatiwa huduma za afya majumbani kwao.

Sauti ya katibu mkuu mendaji

Afisa tarafa ya Geita Cosmas Bayaga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Geita ameiagiza halmashauri ya mji wa Geita kuhakikisha kila kituo cha kutolea huduma za afya kinakuwa na dirisha la wazee kama serikali inavyoelekeza.

Sauti ya afisa tarafa
Cosmas Bayaga, Afisa tarafa Geita. Picha na Edga Rwenduru