Storm FM

Wananchi, mashirika ya kiraia Geita walaani tukio la mtoto albino kuuawa Kagera

18 June 2024, 8:40 pm

Watoto na baadhi ya walimu wakiwa katika maandamano siku ya mtoto wa afrika Nyamigota. Picha na Mrisho Sadick

Kuanza kushika kasi kwa matukio ya watu wenye ualbino kuuawa nakukatwa viungo vyao imewaibua wananchi mkoani Geita

Na Mrisho Sadick:

Wananchi na mashirika ya kiraia mkoani Geita wamelaani vikali tukio la mtoto mwenye ualbino kuuawa na kukatwa viungo vyake vya mwili Mkoani Kagera huku wakiiomba serikali kuongeza nguvu kudhibiti vitendo hivyo vilivyoanza kushika kasi kwa baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa.

Wananchi hao wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Kimkoa katika Kata ya Nyamigota wilayani Geita wameguswa na tukio la Mtoto huyo kuuawa Mkoani Kagera ikiwa zimepita siku chache tu za Mtoto mwingine mwenye ualbino katika Kata ya Katoro wilayani Geita kushambuliwa nakujeruhiwa kwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Baadhi ya watoto na wakazi wa kata ya Nyamigota wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika. Picha na Mrisho Sadick

Mwenyekiti wa baraza la watoto mkoa wa Geita Loys Endrew ametoa rai kwa watoto wote wa mkoa wa Geita kutofumbia macho vitendo vya ukatili nabadala yake watoe taarifa wanapoona vitendo hivyo.

Sauti ya mwenyekiti baraza la watoto Geita
Mwenyekiti wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Geita akizungumzia suala la mtoto mwenye ualbino kuuawa kagera. Picha na Mrisho Sadick

Mwenyekiti wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Geita ambae ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la NELCO Bi Paulina Alex Majogoro kwa niaba ya mashirika yote mkoani humo amelaani vikali tukio hilo huku akiitaka serikali kuongeza nguvu katika ulinzi na usalama wa mtoto.

Sauti ya mkurugenzi NELCO

Akizungumza kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba amesema serikali imejipanga kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo wenye ualbino.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Geita