Msako waganga wanaosababisha mauaji Geita
9 April 2024, 6:01 pm
Matukio ya watu kudaiwa kukamatwa hovyo na wananchi katika kijiji cha Iparamasa Chato yamemuibua Kamanda wa Jeshi la Polisi.
Na Mrisho Sadick – Geita
Jeshi la polisi Mkoani Geita linaendelea kuwasaka nakuwakamata waganga wa tiba asili ambao wanafanya ramli chonganishi katika maeneo mbalimbali mkoani humo ambazo zimekuwa zikileta madhara katika jamii ikiwemo mauaji.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Safia Jongo ametoa kauli hiyo katika kijiji cha Iparamasa wilayani Chato kufuatia malalamiko ya baadhi ya wakazi wa eneo hilo ya uwepo wa vitendo vya kamata kamata.
Awali wakitoa malalamiko mbele ya mkuu wa mkoa wa Geita baadhi ya wakazi wa Kata ya Iparamasa wametaka kufahamu juu ya vitendo vya watu kukamatwa nakupelekwa vituo vya polisi ambavyo viko nje na wilaya hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka wakazi wa eneo hilo kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi kwa kuwafichua waganga wanaoendelea kufanya ramli chonganishi.