Zaidi ya vijiji 5 maji ni changamoto Geita
3 January 2024, 10:27 am
Vijiji vitano vya kata ya Bukondo mkoani Geita havina huduma za maji huku zahanati ya Bukondo inayohudumia vijiji vitano katika kata hiyo ikiwa na watumishi wawili tu.
Na Zubeda Handrish- Geita
Wananchi wa kata ya Bukondo mkoani Geita wamemweleza changamoto zao Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita Bwana Barnabas Mapande alipotembelea Kata hiyo kutatua changamoto za wananchi na kuongeza kuwa hali ya ukosefu wa huduma ya afya na maji safi na salama zisababisha utoaji wa huduma kwa wananchi kukwama, huku wakiiomba serkali kuchukua hatua za haraka ili kuwaondolea kero hizo.
Aidha kuhusu Elimu Diwani wa Kata ya Bukondo Bwana Thomas Turukenzire ameiomba serikali kuwasaidia ujenzi wa daraja linalokwamisha shughuli mbalimbali ikiwamo wanafunzi hasa katika kipindi hiki shule zinakaribia kufunguliwa.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita Bwana Barnabas Mapande amesema Serikali imetoa zaidi Ya Bilioni Mia Moja na ishirini na nane ili kumaliza tatizo la maji safi na salama kwa mkoa wa geita.