Wilaya ya Geita kufanya msako wa wazazi waliotelekeza familia
12 October 2023, 11:05 am
Wakati serikali ikiendelea kupambania haki sawa kwa mtoto wa kike wananchi na wadau wametakiwa kuiunga mkono katika mapambano hayo.
Na Mrisho Sadick:
Watendaji wa Mitaa na Kata wilayani Geita wameagizwa kufanya msako nakuwachukulia hatua kali wazazi na walezi ambao wamewatelekezea familia watoto wao nakuwakosesha haki yao ya msingi ya kupata elimu.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Geita katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa kike duniani katika viwanja vya shule ya Sekondari Nyanza wilayani Geita.
Kwa upande wake msimamizi wa masuala ya jinsia katika mradi wa KAGIS kutoka shirika la Plant Internation Hildegada Mashauri amesema kwasasa jamii imeendelea kuwa na mwamko hususani katika kumsomesha mtoto wa kike kwani hapo awali hali hayo haikuwepo kabisa.
Maadhimisho hayo yameratibiwa na Shirika la Plan International kwa kushirikiana na Rafiki SDO kupitia mradi wa KAGIS unaofadhiliwa na serikali ya watu wa Canada huku wanafunzi na wadau wa kutetea haki za Mtoto wa kike wakisema.