Waliotiririsha maji taka barabarani Geita wapigwa faini
18 August 2023, 6:08 am
Uchafuzi wa mazingira ni kikwazo kwa maendeleo ya mitaa kwani ni chanzo pia cha magonjwa ya mlipuko.
Na Kale Chongela- Geita
Wakazi wawili mmoja akijulikana kwa jina la Mama Nelson wakazi wa Mtaa wa Ujamaa Halmashauri ya Mji wa Geita mkoani Geita, wamepigwa faini ya shilingi laki mbili kila mmoja na uongozi wa serikali ya mtaa huo kwa kosa la kutiririsha maji machafu barabarani kuelekea kwa majirani zao kitendo kilichopelekea majirani hao kwenda kulalamika serikali ya mtaa.
Mtuhumiwa wa uchafuzi huo anaefahamika kama Mama Nelson kutoka mtaa wa Ujamaa na Marry Nkya ni Afisa Mtendaji wa Mtaa huo amesema baada ya kupata malalamiko kutoka kwa Majirani wa wananchi hao aliwaita mara ya kwanza na kuwapa maelekezo ya kuacha kufanya hivyo lakini wamekaidi na kuendelea kutiririsha maji hayo na ndipo ameamua kuwachukulia hatua zaidi na kuwapiga faini ya laki mbili mbili kwa mujibu wa sheria na utaratibu wa halmashauri ya mji wa Geita.