Umoja wa wanawake wilaya ya Geita Kumuenzi JPM kwa kuchapa kazi
5 April 2021, 1:23 pm
Jumuiya ya umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi wilaya ya Geita umesema wanawake watamuenzi Hayati Dkt John Pombe Magufuli kwa kuchapa kazi na kusimamia haki na kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan ili kutimiza maono ya mtangulizi wake.
Tamko hilo limetolewa na Bi Antonia Charles Lubadila mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Geita wakati wa uzinduzi wa kituo cha ushonaji na utengenezaji nguo za batiki kinacho milikiwa na kikundi cha wanawake kata ya katoro mkoani Geita.
Stephania Benjamini na Maimuna Mingisi Madiwani wa viti maalumu katika wilaya ya Geita wamezungumzia kifo cha Hayati Dkt John Pombe Magufuli alivyowabeba akinamama wakati wa uongozi wake na kuwasaidia kukuza uchumi wao na walivyoridhika na uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu wake Dkt Philip Mpango.