Kampuni ya utafiti wa madini yakana kuwalipa fidia wananchi kupisha maeneo yao.
4 April 2021, 2:21 pm
KAMPUNI ya Utafiti wa madini ya Mabangu imekana kuzilipa fidia ya mashamba familia 22 za wakazi wa kijiji cha Nyakafulu wilayani Mbogwe mkoani Geita ili kupisha shughuli za uchimbaji na badala yake imesema malipo iliyowalipa yalikuwa ni kwa ajili ya Usumbufu wa utafiti katika maeneo yao.
Akizungumzia hatua hiyo Meja Mstaafu, Bahati Matala ambae ni Mshauri wa mahusiano ya Jamii wa Kampuni ya Mabangu amesema kampuni hiyo imelazimika kutoa ufafanuzi kutokana na sintofahamu iliyoibuka kati ya Serkali ya wilaya ya Mbogwe na Familia hizo 22 baada ya Serkali ya wilaya ya Mbogwe kuzizuia familia hizo kunufaika na uzalishaji wa madini ya dhahabu yanayopatikana katika mashamba yao.
Miongoni mwa watu wanaodai kuwa ndio wamiliki halali wa mashamba hayo wamesema malipo yaliyofanywa na kampuni ya mabangu yalikuwa ya usumbufu wa kuruhusu kufanyika utafiti katika mashamba yao na siyo fidia ya kupisha shughuli za uchimbani nakwamba kinachofanyika kwasasa nikuminya haki zao.
Martha Mkupasi Mkuu wa wilaya ya Mbogwe hivi karibuni akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alisema Serikali ya wilaya imezizuia familia hizo 22 kunufaika na uzalishaji wa madini ya dhahabu unaopatikana katika mashamba hayo kwa madai kuwa walishalipwa fidia na kampuni ya Utafiti Madini ya Mabangu ili kupisha shughuli za uchimbaji.