Storm FM

Vitendo vya ukatili bado changamoto Geita

19 December 2024, 8:43 pm

Muonekano wa picha ya round abaut ya mjini Geita.Picha na Storm FM

Elimu yahitajika zaidi kwa wananchi ili kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili katika jamii kwakuwa hali bado si shwari.

Na Kale Chongela:

Wakazi wa Geita mjini wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili na madhara yake kwakuwa baadhi ya wananchi wamekuwa na tabia ya kufumbia macho vitendo hivyo kisha kumalizana kindugu bila kujali athari watakazo pata wahanga.

Wametoa wito huo mapema hii leo wakati wakizungumza na Storm FM kwa nyakati tofauti mjini Geita kutokana na kuendelea kwa matukio ya vitendo vya ukatili katika jamii huku wakikemea tabia za baadhi ya watu kumalizana kindugu badala ya kuripo matukio hayo kwa mamlaka husika ili haki itendeke.

Sauti ya wananchi Geita
Muonekano wa mji wa Geita kwa juu. Picha na Storm FM

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi safia Jongo ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuacha tabia ya kufumbia macho vitendo vya ukatili nabadala yake watoe taarifa haraka za vitendo hivyo ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii.

Sauti ya kamanda wa polisi Geita