DC Geita atoa maelekezo ya utendaji kwa wenyeviti
6 December 2024, 4:54 pm
Mkuu wa wilaya ya Geita ametoa mwongozo wa kiutendaji kwa wenyeviti kutoka kata 13 za halmashauri ya mji wa Geita na kata 37 za halmashauri ya wilaya ya Geita.
Na: Ester Mabula – Geita
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba amewasisitiza wenyeviti waliochaguliwa kuzingatia miiko ya kiutendaji na kufanya kazi kwa maslahi ya wananchi ili kuchochea maendeleo katika maeneo yao.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Disemba 05, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa EPZA katika halmashauri ya mji wa Geita Mhe. Komba amewasisitiza kutatua kero za wananchi na kuepuka migongano na wananchi wao.
Akizungumza katika mkutano huo Katibu mwenezi na mafunzo wa CCM wilaya ya Geita Gabriel Nyasilu amewaeleza wenyeviti kufanya kazi kwa bidii ili kuendeleza imani ya Chama kwani imewaamini na kuwapa ridhaa kuweza kusaidia wananchi
Baadhi ya wenyeviti wakizungumza baada ya mkutano huo wameeleza namna walivyopokea maelekezo ya mkuu wa wilaya na kuahidi kuyafanyia kazi
Uchaguzi wa serikali za mitaa ulifanyika Novemba 27, 2024 ambao uluhusisha uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa, vitongoji na vijiji katika mikoa ya Tanzania bara.