Storm FM

Watendaji watumiwa meseji za vitisho Geita

12 November 2024, 7:31 pm

Msimamizi wa uchaguzi akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani Geita mji. Picha na Mrisho Sadick

Joto la uchaguzi wa serikali za mitaa linaendelea kupanda kadri siku zinavyozidi kusogea ambapo katika halmashauri ya mji wa Geita kumedaiwa uwepo wa vitisho kwa watendaji.

Na Mrisho Sadick:

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Geita mjini Yefred Myenzi amekemea vikali tabia ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa katika eneo hilo kuanza kuwatumia meseji za vitisho wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ambao ni watendaji kwa madai yakutoridhika na maamuzi mbalimbali ambayo yanafanywa wasimamizi hao.

Myenzi ametoa kauli hiyo leo Novemba 12,2024 katika kikao cha baraza la madiwa la halmashauri ya mji wa Geita katika ukumbi wa EPZA Bombambili Geita mjini ambapo amewataka viongozi wa vyama vya siasa katika eneo hilo kuacha tabia ya kuwatisha watendaji nabadala yake wazingatie misingi ya utawala bora , sheria na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa kama kuna mahali hawajatendewa haki.

Madiwani na wajumbe mbalimbali wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Geita. Picha na Mrisho Sadick

Amesema ofisi yake imeendelea na taratibu mbalimbali za uchaguzi nakwamba kwa halmashauri ya mji Geita vyama saba vya siasa vimejitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo na iwapo kuna mgombea hajaridhika na maamuzi ya mchakato wa uteuzi anatakiwa kuwasilisha malalamiko yake kuanzia Novemba 10 hadi 13 mwaka huu.

Sauti ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Geita
Wajumbe mbalimbali wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Geita. Picha na Mrisho Sadick