Wananchi 226 walipwa fidia wilayani Nyang’hwale
12 November 2024, 3:28 pm
Jumla ya wananchi 226 katika kata ya Mwingiro wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita wamelipwa fidia ya zaidi ya shilingi bilioni 7.2 kutokana na maeneo yao kuchukuliwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa zaidi ya miaka 20 .
Na: Kale Chongela – Geita
Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita Bw. Azza Mtaita akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 12, 2024 amesema maeneo hayo ya wanachi yalichukuliwa na mgodi huo kwa zaidi ya miaka 20 bila wananchi kunufaika chochote ndipo TAKUKURU wakaanza kufanya ufuatiliaji.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2024 jumla ya kesi 15 zinazohusu Rushwa ziliendelea katika mahakama mbalimbali ndani ya mkoa wa Geita.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa TAKUKURU imejipanga kuendelea kudhibiti vitendo vya Rushwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.