Tutumie nishati mbadala kuokoa Mazingira
4 June 2021, 9:41 pm
Jamii katika halmashauri ya mji wa Geita mkoani Geita imetakiwa kutumia nishati mbadala kwa matumizi ya majumbani na sehemu za kazi ili kuondokana na changamoto ya ukataji wa miti na utupaji wa taka hovyo.
Rai hiyo imetolewa na afisa mazingira wa halmashauri ya mji wa Geita Bi Bingai Charles katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo kwa halmashauri ya mji wa Geita yamefanyika katika viwanja vya Gedeco mjini Geita.
BiĀ Mpelwa James ni afisa mazingira kutoka halmashauri ya mji wa Geita ametumia maadhimisho hayo kuikumbusha jamii kuendelea kuhifadhi mazingira kwa kutumia nishati mbadala.
Maadhimisho ya siku ya mazingira dunia huadhimishwa kila June 5 ya kila mwaka na kimkoa yatafanyika wilayani chato huku yakiongozwa na Kaulimbiu ya tutumie nishati mbadala kuongoa mfumo ikolojia.