Storm FM

Bei ya nyanya mjini Geita yapanda, wauzaji wafunguka

23 October 2024, 1:54 am

Picha ya muonekano wa zao la nyanya kwaajili ya kuuza kwa wateja. Picha kutoka maktaba

Zao la nyanya ni miongoni mwa mazao muhimu ya kilimo nchini Tanzania, likiwa na umuhimu mkubwa katika chakula na biashara.

Na: Kale Chongela – Geita

Baadhi ya wauzaji wa nyanya katika soko la asubuhi Nyankumbu katika halmashauri ya mji wa Geita wameeleza bei ya zao hilo kwa sasa imepanda hali ambayo imesababishwa na mvua inayoendelea kunyesha nchini.

Wameeleza kuwa licha ya zao hilo kupatikana kwa wingi bei yake imekuwa ikipanda bei na kubadilika .

Sauti ya wauzaji wa nyanya

Mwenyekiti wa wafanybiashara wa nyanya katika soko hilo ameeleza kuwa hiyo imekuwa ni fursa kwa wafanyabiashara kuweza kupata faida kupitia kilimo cha zao hilo.

Sauti ya mwenyekiti

Afisa kilimo kutoka halmashauri ya mji wa Geita akizungumza kwa njia ya simu amekiri kuwa msimu wa mvua hupelekea bei ya zao hilo kupanda.

Sauti ya Afisa kilimo