Daraja la Butobela-Bukoli kukamilika mwezi Juni
10 May 2024, 2:32 am
Kwa zaidi ya miaka 20 daraja la Butobela-Bukoli limekuwa ni kitendawili jambo ambalo lilikuwa likilazimu wananchi kutumia zaidi ya KM 40 kufika Bukoli kwa kutumia njia ya Kahama.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Ujenzi wa daraja linalounganisha kata ya Bukoli na Butobela ambalo ujenzi wake ulianza mwanzoni mwa mwezi aprili mwaka huu linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi juni na kuanza kutumika.
Kauli hiyo imetolewa na mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa daraja hilo baada ya Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhandisi Tumaini Magesa kutembelea na kukagua mwenendo wa ujenzi wa daraja hilo.
Aidha Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhandisi Tumaini Magesa amebainisha kuwa wananchi wa kata hizo wameathirika kwa kipindi cha miaka 20 sasa kutokana na ubovu wa daraja hilo ambapo amesema daraja hilo likikamilika litaondoa changamoto ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili wananchi Bukoli na Butobela.
Mhandisi Magesa ameongeza kuwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani ametoa zaidi ya milioni 200 kwaajili ya ujenzi wa daraja hilo.