Ngo’mbe wawili wamekufa baada ya kunywa maji yenye sumu Geita
23 April 2021, 6:07 pm
Na Kale Chongela:
Ng’ombe wawili wamekufa baada ya kunywa maji yenye sumu kutokana na kutapakaa kwa maji yenye sumu yanayo toka katika eneo la uchenjuaji wa madini ya dhahabu katika mtaa wa Samina Kata ya Mtakuja Halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita.
Akizungumza na Storm Fm kwa njia ya simu Daktari wa mifugo wa Halmashauri ya mji wa Geita Jasson Mutayabarwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo baada ya uchunguzi wa sampuli ya maji hayo ambapo amebaini sumu kuathiri baadhi ya viungo vya ng’ombe hao nakuwasababishia kifo.
Mmiliki wa ng’ombe waliokufa Bw Godson Luvugo ambaye ni mkazi wa eneo la Samina ameuomba uongozi wa ofisi ya madini na kata ya Mtakuja kutafta namna ya kutatua changamoto kwani sio mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea kwenye kata hiyo.
Nae Afisa madini Mkoa wa Geita Bw Daniely Mapunda amesema atahakikisha anasimamia sheria kwa mujibu wa taratibu na kanuni ambazo zinatakiwa kufuatwa na wawekezaji eneo la makazi ya watu ili kuepukana na migogoro isio kuwa ya lazima.