Waliomteka mtoto na kudai milioni 4 watiwa mbaroni Mbogwe
19 January 2024, 1:29 pm
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limejipanga kukabiliana na matukio ya ukatili kwa watoto ikiwemo ya kubakwa na kuuawa.
Na Mrisho Shabani – Geita
Jeshi la polisi Mkoa wa Geita limewakamata watu watatu wilayani Mbogwe kwa tuhuma za kumteka mtoto mwenye umri wa miaka minneĀ kisha watekaji hao wakaomba milioni nne ili wamwachie.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishna msaidizi wa polisi ACP Safia Jongo amethibitisha kukamatwa kwa watu hao wakati akizungumza na waandishi wa habari kutokana na kushamiri kwa matukio ya watoto kuibiwa , kubakwa na kuuawa.
Katika hatua nyingine kamanda Jongo amesema Jeshi hilo limeanza msako wa waganga wanaofanya ramli chonganishi ikiwemo kuwataka wateja wao kubaka au kufanya mauaji ya watoto ili wapate utajiri.
Amewataka wananchi kuwa makini na watoto wao kwakuwa baadhi ya wazazi wamesahau wajibu wao wa malezi hali ambayo inaleta changamoto kubwa.