EWURA kutokomeza mafuta ya kupimwa kwa chupa vijijini
23 September 2023, 1:44 pm
Changamoto ya wauza mafuta ya petroli na dizeli vijijini kuuza kwenye chuma imekuwa kubwa kiasi cha EWURA kulitafutia ufumbuzi.
Na Zubeda Handrish- Geita
Katika kuhakikisha wafanyabishara na wasafirishaji vijijini wanaondokana na mafuta ya kupima kwenye chupa (makopo), mamlaka ya usimamizi wa nishati ya mafuta na Maji nchini EWURA imetunga Sheria na kanuni ambayo imeruhusu mtu yoyote kujenga kituo cha mafuta maeneo ya vijijini nakuuza mafuta kwa kwa bei elekezi.
Hayo yamesemwa na meneja wa Ewura Kanda ya ziwa George Mhina Mjini. Geita katika kongamano ya taasisi mbalimbali za serikali zinahusika na utoaji wa leseni kwa wafanyabishara na wachimbaji wa madini.
Mhina amesema kwa Sheria ya Sasa ujenzi wa kituo Cha kuuzia mafuta vijijini mtu anaruhiwa kujenga kwa Shillingi Million 50 lengo likiwa kutomeza mafuta ya kupima.