Walazimika kuanzisha kituo cha Polisi kukabiliana na uhalifu
15 April 2021, 6:08 pm
Na Mrisho Sadick:
Kutokana nakushamili kwa vitendo vya uhalifu katika kata ya Nyankumbu mjini Geita wananchi na viongozi wa eneo hilo wamelazimika kuanzisha kituo kidogo cha polisi ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Wakizungumza katika eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi, na kituo kidogo cha muda baadhi ya wakazi wa kata hiyo wamepongeza kuanzishwa kwa kituo hicho kwakusema kuwa kitasaidia kupunguza vitendo vya uhalifu katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa uwanja kilipo kituo hicho Bw Enos Chelehan amesema kilichowasukuma kuanzisha kituo hicho nitukio la mlinzi katika mtaa huo kuuawa naduka kuteketea kwa moto nakwamba kituo hicho kitakuwa msaada kwa wakazi wa kata hiyo.
Diwani wa kata ya Nyankumbu Bw Jonh Mapesa amesema kwasasa wameandaa kituo cha muda wakati wakijipanga kujenga jengo la kituo kwa kushirikiana na wananchi.