Wafugaji wa Nyuki Geita watakiwa kufuga kisasa
28 August 2023, 1:34 pm
Ufugaji wa Nyuki umeendelea kuongezeka kwa kasi Mkoani Geita na maeneo mbalimbali huku idadi kubwa ya watu wanaoingia kwenye ufugaji huo wakiwa hawajui kanuni za ufugaji.
Na Kale Chongela:
Wafugaji wa Nyuki katika Kata ya Buhalahala wilayani Geita Mkoani Geita wametakiwa kufuata kanuni bora za ufugaji ili kuepuka nyuki hao kuleta madhara kwa watu.
Rai hiyo imetolewa na Mtaalam wa Sayansi ya maisha ya Nyuki Bw Mbelwa Petro kutoka shamba la Nyuki lililopo Biharamulo Mkoani Kagera katiKa eneo la ufugaji wa Nyuki Idara ya Vijana wa kanisa la AICT Shilabela ambapo amesema ufugaji bora lazima uzingatie kilomita 2 kutoka katika makazi ya watu.
Aidha ameongeza kuwa katika kuendelea kutatua changamoto ya ufugaji wa nyuki holela wanaendelea kutoa elimu ya ufugaji wa kisasa wa nyuki.
Kwa upande wake Meneja wa kituo cha Safina Idara ya Vijana Scola Charles Njige amesema kuna umuhimu wa ufugaji wa Nyuki kwani wamekuwa wakinufaika na uwepo wa asali halisi.